Magoha awaonya wazazi dhidi ya mitihani gushi

Mwenyekiti wa bodi ya baraza la mitihani ya kitaifa nchini, George Magoha, amewatahadharisha wanafunzi na wazazi dhidi ya kuhadaiwa kununua karatasi bandia za mitihani ya kitaifa. Magoha ambaye alikuwa katika kaunti ya Migori kuanzisha rasmi mitihani ya kitaifa aliwaonya wale wanaonuia kuwahadaa watahiniwa kwa kuwauzia karatasi bandia za mitihani hiyo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria. Magoha ambaye alikuwa akiongea wakati wa usambazaji wa karatasi za mtihani wa KCPE katika afisi za kamishna wa kaunti hiyo aliitaka jamii kuhakikisha mazingira bora kwa watahiniwa kufanya mitihani yao. Magoha alisisitiza haja ya watahiniwa kutojihusisha na udanganyifu katika mitihani.Onyo hilo limetolewa huku A�mitihani ikikosa kuanza katika baadhi ya maeneo kwa wakati ufaao kwa sababu ya changamoto za mipangilio.