Magavana watatu kuapishwa leo

Sherehe za kuwaapisha magavana watatu akiwemo wa Bomet, Kirinyaga na Mombasa zinaendelea kwa sasa. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kumuapisha gavana mteule wa Bomet, Joyce Laboso. Naibu wake William RutoA�naye anahudhuria hafla ya uapisho wa gavana mteule wa Kirinyaga, Anne Waiguru. Gavana wa Bomet anayeondoka, Isaac Ruto aliyeshindwa katika kinyanganyiro hicho cha ugavana, alisema atahudhuria sherehe ya kumuapisha Laboso. Viongozi wote wawili awameahidi kujitolea kuhakikisha umoja wa wakazi wa Bomet, wakisema uchaguzi umepita na sasa kinachopaswa kuangaziwa ni Maendeleo. Naye gavana mteule wa Mombasa, Ali Hassan Joho pia aliapishwa katika sherehe iliyohudhuliwa na mgombeaji urais na muungano wa NASA, Raila Odinga. Katika hotuba yake, Joho alikariri kujitolea kwake kuwatumikia wakazi waA� Mombasa. A�Siku ya Jumatatu, magavana 31 waliapishwa ambapo waliahidi kuhakikisha mabadiliko katika kaunti zao, wengi wao wakiutaja ufisadi kuwa kikwazo kikubwa cha Maendeleo.A� A�