Magavana watatu kati ya wanasiasa wanane huenda wakafutiliwa mbali kwenye uchaguzi ujao

Magavana watatu ni miongoni mwa wanasiasa wanane ambao huenda wakafutiliwa mbali kwenye uchaguzi mkuu ujao iwapo hawatalipa jumla ya shilingi milioni 10.5 kufikia leo jioni. Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC jana iliwatoza faini wanasiasa kwa kukiuka kanuni za uchaguzi na kufikisha milioni 15 kiwnago chaA� jumla cha pesa zinazotozwa wanasiasa hao.A� Gavana wa Bungoma Ken Lusaka wa chama chaA� Jubilee ametozwa shilingi milioni moja kwa mara ya pili katika muda wa chini ya mwezi mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuruhusu msururu wa pili wa ghasia dhidi ya mpinzani wake mkuu wa Wycliffe Wangamati wa chama cha Ford Kenya. Mwenzake waA� Mandera Ali Roba pia ametozwa faini ya kiwango hicho kutokana na rabsha zilizozuka wakati rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akihutubia mikutano katika kaunti hiyo . Mpinzani wake wa chama cha Economic Freedom Hassan Noor ameagizwa kulipa shilingi milioni tatu kutokana na rabsha hizo. Katika kaunti yaA� Marsabit, gavana Ukur Yatani wa chama chaA� Frontier Alliance vile vile ameagizwa kulipa shilingi milioni tatu kutokana na msururu wa ghasia zilizoshuhudiwa tarehe 26 mwezi Julai wakati wa ziara ya rais Uhuru Kenyatta katika kaunti hiyo. Mpinzani wake wa chama chaA� JubileeA� Mohamed Mohamoud atalazimika kulipa shilingi milioni moja kutokana na ghasia hizo. Tume hiyo pia imetoza faini wabunge watano kwa makosa yaliyotokana na rabsha na kutumia vyama vya mirengo mbali mbali ilhali wao ni wagombeaji huru.