Magavana Watahadhari Wakazi Wa Malindi Dhidi Ya Wanunuzi Wa Kura

Gavana wa Kilifi, Amason Kingi na mwenzake wa Mombasa, Ali Hassan Joho wamehimiza wakazi wa eneo la Malindi wajihadhari na baadhi ya watu wanaozunguka katika eneo hilo wakinunua kadi za kupigia kura. Wakimfanyia kampeni mgombeaji wa chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi, magavana hao waliwatahadharisha wakazi dhidi ya kudanganywa na watu wasiojali maslahi yao. Zikiwa zimesalia siku saba tu kabla ya kinyang’anyiro hicho, magavana hao wawili walitaka wakazi wa eneo hilo kumchagua mgombeaji wa chama cha ODM, Willy Mtengo ambaye walisema anafahamu matakwa yao. Mtengo anakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Jubilee Alliance,Philip Charo.