Magavana Wampasha Uhuru Kuhusu Kuonyesha Dhamira Kuhusu Suala la Ugatuzi

Mkutano wa tano wa ushirikishi wa serikali ya taifa na zile za kaunti unaoandaliwa katika hoteli ya Sagana huko Nyeri uliendelea leo kwa siku ya pili. Mkutano huo wa siku mbili uliozinduliwa jana na rais Uhuru Kenyatta leo utashirikisha wanahabari baada ya kikao cha faragha kuandaliwa jana. Mkutano huo unatarajiwa kukadiria ufanisi ambao umeafikiwa kupitia mfumo wa ugatuzi, kwa kuangazia taarifa za kamati mbali mbali. Katika mkutano huo, ufanisi pamoja na changamoto za mfumo wa ugatuzi, vitaangaziwa. Aidha mkutano huo utajadilia ripoti mbali mbali za usimamizi wa pesa zikiwemo sheria za utozaji ushuru zaidi ya mara moja, mfumo wa uhifadhi habari za kifedha-IFMIS, matumizi ya fedha na usimamizi wa ruzuku za masharti. Kilele cha mkutano huo unaotarajiwa kumalizika leo, kitakuwa hotuba ya rais kwa taifa kuhusiana na swala la ugatuzi.