Magavana walitaka bunge la senate kupinga kupunguza pesa zinazotolewa kwa kaunti

Magavana wamelitaka bunge la Senate kupinga juhudi zozote za wizara ya fedha za kupunguza pesa zinazotolewa kwa kaunti. Magavana hao wamesema pendekezo la wizara hiyo la kupunguza pesa hizo kwa shilingi bilioni- 18 litaathiri vibaya utoaji huduma katika kaunti. Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi,A�mwenyekiti wa baraza la magavana nchiniA�A�Josphat Nanok alisema kuwa tayari serikali za kaunti zinakumbwa na uhaba wa kifedha baada ya kupokea asili mia 33 pekee ya mgao wao wa kifedhaA�na hivyo kupunguza kiasi hicho kutatatiza utekelezaji miradi ya maeneleo.A�Nanok pia alisema kuwa wizara ya fedha haijashauriana na kaunti kuhusu kupunguza pesa hizo. Gavana huyo wa Turkana alisema kuwaA�mipango hiyo ya wizara ya fedha haiwezi kutekelezwa kabla ya kurekebishwa kwa sheria.A�A�Wizara ya fedha siku ya Jumatano ilitoa pendekezo kwaA�Senate kuhusu kurekebisha sheria hiyo na kupunguza pesa zinazotolewa kwa kaunti kwa shilingi bilioni-18 kutoka shilingi bilioni-302 hadi shilingi bilioni-284 kutokana na kupungua kwa mapato ya nchi