Magavana wahimiza wauguzi kurejea kazini kufikia tarehe 8

Magavana wamesisitiza kwamba makubaliano ya pamoja yaliofikiwa kuhusiana na mishahara ya wauguzi, hayawezi kutekelezwa jinsi yalivyo. Magavana hao pia wamekariri kwamba mgomo huo wa wauguzi ni haramu kwa vile walianza kugoma kabla mashauriano kukamilika. Ni kutokana na sababu hiyo, magavana hao wamewataka wauguzi hao kurejea kazini kufikia tarehe nane mwezi huu au wafutwe kazi mara moja. Wakiongea wakati wa kikao cha kuwakaribisha magavana wapya, mwenyekiti wa sasa wa baraza la magavana nchiniA�A�Josphat Nanok alisema magavana hao wamefanya kila wawezalo kutatua mzozo huo. Nanok aliwahakikishia wauguzi hao kwamba serikali za kaunti zitaondolea mbali barua za kinidhamu ambazo zilikuwa zimetowelaA�A�kwa wauguzi hao kabla ya tarehe nane mwezi huu, na pia watalipwa mishahara yao kuanzia wakati walipoanza kugoma, endapo watarejea kazini. Hatahivyo wauguzi wamekariri kwamba hawatarejea kazini hadi matakwa yao yatakapotekelezwa kikamilifu. Wauguzi wamekuwa wakigoma tangu tarehe tano mwezi juni.