Magavana zaidi waapishwa leo

Alex Tolgos gavana mteule wa kaunti ya Elgeyo-Marakwet aliapishwa leo na kuahidi kuleta mabadiliko yatakayowafaidi wakazi. Naye gavana mteule wa Kisumu, Anyang Nyongo alifichua mikakati dhabiti aliyosema yatabadilisha kaunti hiyo katika muda wa siku 100. Huko Nyeri Dr Wahome Gakuru aliapishwa kuwa gavana wa tatu wa kaunti hiyo kwenye sherehe iliyohudhuriwa na waziri wa teknolojia ya mawasiliano Joe Mucheru. Magavana wengine walioapishwa leo ni pamoja na Francis Kimemia wa Nyandarua, Salim Mvurya wa Kwale, Granton Samboja wa Taita Taveta, Amason Kingi wa Kilifi, gavana wa kaunti ya Garissa Ali Korane, gavana wa Siaya Cornel Rasanga, gavana wa Wajir, Mohamed Abdi, Samuel Tunai wa Narok, Jackson Mandago wa Uasin Gishu, gavana wa Nandi Stephen Kipyegon arap Sang na wengineo. Gavana Joyce Laboso aliyembwaga Isaac Ruto huko Bomet ataapishwa kesho kwenye sherehe itakayohudhuria na rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto.