Mafuriko Nigeria yazua hofu ya kuzuka kwa maradhi

Kituo kikuu cha kudhibiti magonjwa nchini Nigeria-CDC kimetoa tahadhari ya kuzuka maradhi kutokana na mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea  nchini humo.

Tahadhari imetangazwa katika majimbo manne,ambako zaidi ya watu 100 waliangamia katikia kipindi cha majuma mawili kutokana na mafuriko na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu kama vile kipindupindu, ugonjwa wa kuhara damu na homa ya matumbo.

Kituo hicho kimetoa tahadhari,ikiwemo ili ya kutokula vyakula hadharani na kuwataka watu kuzingatia usafi wanapotayarisha chakula.Hata hivyo wakazi wa kijiji cha Egagi,katika jimbo la Niger  hawana la kufanya ila kuyatumia maji ya mafuriko hayo kwa kuwa hawana maji mengine kwa matumizi ya kawaida.