Maelfu ya Maafisa wa NYS Kufuzu Kesho

Rais Uhuru Kenyatta kesho ataongoza sherehe ya kufuzu kwa zaidi ya makurutu elfu 10 katika taasisi ya shirika la huduma za vijana kwa taifa ,NYS. Waziri wa Utumishi wa Umma, Vijana na Maswala ya Jinsia, Sicily Kariuki amesema sherehe hiyo itahusisha makurutu 7,903-wanaume na 2,848 wanawake ambao wamekamilisha mafunzo yao katika taasisi hiyo.A� Makuruti hao kupitia mradi wa kuwezeshaji vijana, wanatarajiwa kupelekwa katika sehemu mbali mbali za nchi kusimamia ujenzi wa mabwawa, barabara, shughuli za uboreshaji mitaa ya mabanda, kusimamia shughuli za trafiki na vituo vya kilimo. Hii itakuwa sherehe ya pili ya aina hiyo mwaka huu, baada ya wa kwanza kuandaliwa mwezi Aprili mwaka huu ambapo makurutu 9,031 walifuzu. Hatua hiyo inafikisha takriban makurutu elfu 20 wa kiume na kike ambao wamefuzu mwaka huu. Kabla ya sherehe hiyo, rais Kenyatta anatarajiwa kuzuru na kuzindua kambi 10 mpya katika taasisi ya NYS ya Gilgil itakayotoa hifadhi kwa makurutu elfu 9.A�A�