Maduka Ya Jumla Ya Uchumi Huenda Yakafungwa Kutokana Na Madeni

Maduka ya jumla ya Uchumi huenda yakafungwa kutokana na madeni baada ya kushindwa katika awamu ya kwanza ya kesi ya kuzuia wadeni kuyafilisha maduka hayo.A�Hatma ya maduka hayo ambayo ndio ya zamani zaidi hapa nchini, iko katika shera ya ufilisi nambari 18 za mwaka 2015 ambazo hazijatekelezwa kikamilifu na bunge.A�A�Aidha maduka hayo yalitegemea ombi la kampuni ya Blue Bird Aviation ambapoA�jaji Eric Ogola wa Mahakama kuu aliamua kwamba sheria za zamani za kampuni haziwezi kutumiwa kufunga kampuni hadi bunge litakapotisha kanuni ya kufunga kampuni kupitia sheria za ufilisi. Hata hivyo, jaji Farah Amin wa Mahakama kuu aliamua kwamba maduka ya Uchumi hayawezi kutegemea ombi hilo kwani wadeni wake walianzisha mchakato wa kuyafilisisha maduka hayo kabla ya sheria hiyo kubadilika.A�A�A�Kesi hiyo itatajwa tarehe 2 mwezi Julai.A�