Madereva wa Teksi wa Kampuni ya Uber Wapewa Kauli ya Mwisho

 

Serikali imepewa makataa ya siku saba kusimamisha huduma za teksi za kampuni ya Uber la sivyo kutakuwa na mzozo katika sekta ya uchukuzi. Akiwahutubia wanahabari baada ya kuandaa mkutano, msemaji wa chama cha wenye teksi hapa nchini Mwangi Mubia alisema kusitishwa kwa huduma za teksi za Uber ndilo suluhisho la pekee. Aliwatetea wanachama wake dhidi ya madai kwamba wanawashambulia madereva wa teksi za UBER na badala yake akasema wao ndio waathiriwa wa mashambulizi hayo. Mzozo huo unatokana na madai kwamba teksi za UBER hulipisha nauli nafuu na kuwapokonya biashara wenye teksi za kawaida.