Madaktari Waapa Kutorudi Kazini

Madaktari wanaogoma wamesisitiza kuwa hawatarudi kazini hadi serikali itakapotia saini mkataba wa makubaliano.MadaktariA�A�haoA�A�hata hivyoA�A�wanasema wako tayari kuendelea kushauriana na serikali ili kuafikiana kuhusu maswala chache yanayoibua utata, ili kumaliza mgomo huo ambao umedumu kwa miezi mitatu sasa.Lakini katibu mkuu wa chama cha madaktari na watalaamu wa meno Dr Ouma Oluga kwenye kitandazi chake cha twitaA�A�ameelezea kughadhabishwa na kwake, na kile ametaja kuwa vitisho kutoka kwa serikali,akisema madaktari hawapigani na serikali, bali wanashinikizaA�A�kuboresha kwa sekta ya afya hapa nchiniA�A�kwa jumla, kwa manufaa ya Wakenya wote.A�A�Wakati huo huoA�mwenyekiti wa chama cha madaktari a��KMA Jacqueline Kitulu amevikosoa vyombo vya habari kwa kutoa habari za kupotosha kuhusu nia ya mgomo wa madaktari.Alisema vyombo vya habari vinaangazia tu swala la nyongeza ya mshahara, ilhali kuna maswala mengine muhimu yanayoshinikizwa na madaktari kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.Kitulu amesema hayo huku serikali ya kitaifa na za kaunti zikiendelea kuwafuta kazi madaktari waliopuuza agizo la kurejea kazini.Hadi sasa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imewafuta kazi madaktari 12,huku hospitali nyingine kadhaa pia zikijiandaa kufanya hivyo.