Macharia ajiunga na kilabu cha Koikheti Poti

Aliyekuwa mchezaji wa shule ya upili ya Laiser Hill, John Macharia, amejiunga na kilabu chaA� Kolkheti Poti nchini GeorgiaA� juma moja tu baada ya Mkenya mwengine,A� Amos Nondi,A� kusajiliwa na kilabu hicho kwa mkataba wa miaka mitatu. Wachezaji hao wawili walielekea Georgia jana kufanyiwa uchunguzi wa kiafya, kabla ya kutia saini mikataba yao kilabuni. Kilabu hicho kimethibitisha kuwa Nondi atakuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambapo atajiunga na Mkenya mwenzake aliyekuwa akiichezea timu ya Gor Mahia, Eric Ouma.A� MachariaA�A� ambayeA� atatia saini mkataba wa miaka mitatu, atakuwaA� kwenye kikosi cha chipukizi cha timu ya Kolketi. Anatarajiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza mara moja na atapewa nafasi katika kikosi cha kwanza iwapo atafanya vyema. Kikosi cha chipukizi cha Poti ambachoA� Macharia amejiunga nacho kilimaliza katika nafasi ya 12 kwenye ligi ya chipukizi nchini humoA� msimu waA� mwaka 2015/16.