Maandamano Yasababisha Wanafunzi 40 Kufukuzwa Chuoni

Wanafunzi 40 wa chuo kikuu cha Chuka wamefukuzwa kabisa kwenye chuo kikuu hicho baada ya kubainika kuwa walihusika katika maandamano yaliyosababisha uharibifu wa mali ya thamani ya shilingi milioni 1.6 ya chuo kikuu hicho. A�Akiwahutubia wanahabari mjini A�Chuka, Prof. A�Erastus Njoka, amesema kamati ya nidhamu ya chuo kikuu hicho ilibaini kuwa wanafunzi hao ndio waliowachochea wanafunzi wengine kuandamana baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa chama cha wanafunzi wa chuo kikuu hicho. Prof. Njoka amesema inasikitisha kuwa baadhi ya viongozi wa kisiasa walifadhili wanafunzi kuzua fujo . Hata hivyo amewataka wanafunzi waliofukuzwa chuoni kuzingatia A�taratibu za chuo kikuu hicho na kukata rufaa kwa kamati hiyo ya nidhamu kabla ya kutafuta suluhu ya mahakama kwani baadhi yao wamewasilisha swala hilo mahakamani.