Maandamano Venezuela dhidi ya serikali ya rais Nicolas Maduro

Wabunge na viongozi wa upinzni nchini Venzuela wamefanya maandamano dhidi ya serikali ya rais Nicolas Maduro wakiwa wamepanda kwenye mabasi na treni katika mji mkuu waA� nchi hiyo Caracas.Waandamanaji hao wanalenga kuepuka vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama katika juhudi za kukabiliana na walinda usalama.Wakereketwa pia walipanga kuzuru makao makuu ya tume ya kitaifa ya uchaguzi,ambayo upinzani unashutumu kwa kuipendelea serikali ya rais Maduro,ambayo imelaumiwa kwa kutumia mabavu kushinikiza sera zake. Waandamanaji hao walibeba mabango ya kushutumu utawala wa ki-imla wa raios Maduro.Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa waandamani kuyafikia majengo ya taasisi hiyo.Awali maandamano kama hayo yalizimwa kabla ya kuenea.Wapinzani wa Maduro wamekuwa wakifanya maandamano na mikutano ya hadhara kwa miezi miwili iliopita ambayo yamekuwa yakitibuliwa na polisi na wanajeshi,ambvapo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 71.Wapinzani wa rais Maduro wanadai kuwa anataka kubuni kikundi maalum katika bunge la nchi hiyo ifikapo tarehe 30 mwezi Julai ili kujidumisha mamlakani na washirika wake wa kisoshalisti.Maduro ambaye alichaguliwa baada ya kifo cha mfadhili na mtangulizi wake Hugo Chavez mnamo mwaka wa 2013 amesema kuwa maandamano hayo yamedhamiriwa kuangusha utawala wake na kuushutumu upinzani kwa kusababisha vifo vya raia wengi kwenye ghasia.Maduro amedai kuwa baraza jipya la bunge la nchi hiyo analotarajia kubuni litaisaidia nchi hiyo kukabiliana na hali mbaya ya uchumi inayolikumba taifa hilo.