Maandamano katika Jimbo La Chicago Nchini Marekani Yazuia Mkutano wa Donald Trump

Mkutano wa mgombea uteuzi wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump katika jimbo la Chicago umeahirishwa kufwatia maandamano.

Mkutano huo uliahirishwa kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wa usalama katika eneo hilo.

Mamia ya waandamanaji hao wengi wao asilia ya kiafrika na Latino walighadhabishwa na matamshi ya Trump kuwahusu wahamiaji nchini humo.

Wakosoaji wa Trump wameshutumu kwa kuchochea taharuki kwenye kampeini zake.Mnamo mwaka 1968 ghasia zilikumba uteuzi wa chama cha Democrats katika jimbo hilo hilo ,ulioandaliwa wakati ambapo kulikuwa na mgawanyiko nchini humo kuhusu vita vya Vietnam.Ghasia hizo zimejiri siku chache tu kabla ya kuandaliwa uteuzi wa mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na Missouri tarehe 15 mwezi huu ,huku Trump akiwa kifua mbele katika uteuzi wa chama cha Repiblican.