Maandalizi ya sherehe za Madaraka yakamilika Nyeri

Matayarisho ya sherehe za mwaka huu za siku kuu ya Madaraka zitakazofanyika katka kaunti ya Nyeri siku ya Alhamisi yamekamilika. Tukio hilo litakuwa la tatu kufanyika nje ya Nairobi baada ya kufanyika katika kaunti za Machakos na Nakuru. Akiwahutubia wanahabari katika uwanja wa maonyesho wa Kabiruini ambako tukio hilo litafanyika Mratibu wa eneo la kati, Ann Nga��etich alitoa wito kwa wakenya wajitokeze kwa wingi kwa sherehe hizo zitakazoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Zaidi ya shilingi milioni 70 zimetumika kuukarabati uwanja huo kabla ya tukio hilo la Juni Mosi. Nga��etich aliwahakikishia wageni kuhusu usalama wao akisema maafisa wa usalama wako macho na wamepelekwa kuhakikisha kuwa wanafurahia tukio hilo bila bughdha. Aidha alisema kwamba Vijana wa shirika la huduma kwa taifa NYS pia watapelekwa kusaidiana na maafisa wa usalama na kwamba milango yote ya kuingilia eneo hilo imewekwa alama za kuwaongoza wageni.

Wakati huo huo Nga��etich alisema matayarisho yamefanywa kuhudumia magari yanayongia katika kaunti hiyo ili kupunguza misongamano.