Maajenti wa kupakia na kupakua mizigo watishia Kugoma

Baadhi ya maajenti wa kupakia na kupakua mizigo mjini Mombasa na Nairobi wametishia kulemaza shughuli huku wakishinikiza kuongezwa muda wa matumizi ya leseni zao bila masharti ambazo muda wao ulikamilika mwezi Disemba. Hata hvyo mwenyekiti wa tawi la Mombasa la chama cha maajenti wa kupakia na kupakua mizigo hapa nchini KIFWA Eric Gitonga ametoa wito wa utulivu na kuwahakikishia wanachama wa chama hicho kuwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru hapa nchini KRA itaongeza muda wa kutumika kwa leseni zao kufikia mwezi Aprili. Gitonga aliye pia naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha KIFWA amesema wamewasilisha tayari orodha ya leseni 1100 za wahudumu wa Nairobi na Mombasa kwa halmashauri ya KRA ili kufanyiwa utathmini. Ametoa wito wa kuwa na subira akisema halmashauri hiyo inatayarisha stakabadhi muhimu katika juhudi za kukabiliana na visa vya udanganyifu na kulainsha huduma za sekta ya upakiaji na upakuaji wa mizigo. Gitonga amepuzilia mbali hofu miongoni mwa wadau kuwa halmashauri ya KRA inaleta masharti mapya kwa lengo la kuwafurusha kwenye kazi hiyo.

A�