Maafisa watatu wa kaunti ya Tana River wauawa na wanaoshukiwa kuwa Al Shabaab

Maafisa watatu wa serikali ya kaunti ya Tana River akiwemo afisa mkuu wa ujenzi katika kaunti hiyo waliuawa jana usiku na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab. Maafisa hao watatu walikumbana na mauti waliposhambuliwa katika sehemu ya Nyongoro kwenye mpaka kati ya kaunti za Tana River naA� Lamu. Msako dhidi ya washambulizi hao unaendelea. Miili ya waathiriwa hao ilichomeka kiasi cha kuweza kutambuliwa. Wanamgambo hao walifyatulia risasi basi moja lililokuwa safarini kwenda Kipini na kuliteketeza mwendo wa saa tisa alasiri. Miili hiyo imehifadhiliwa katika hospitali ya Malindi Star. Watu wanne walinusurika kwenye shambulizi hilo wakiwa na majeraha ya risasi na wanatibiwa katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi ambako walipelekwa na maafisa wa shirika la msalaba mwekundu hapa nchini. Shambulizi hilo lilijiri licha ya amri ya kutotoka nje usiku hadi alfajiri kudumishwa katika kaunti za Lamu na Tana River kufuatia msururu wa visa vya utovu wa usalama ambapo katibu katika wizara ya ardhi Mariam El Mawwy alishambuliwa.