Maafisa wa uchaguzi wachunguza kuwepo kwa polisi katika vituo vya kupiga kura nchini Lesotho

Maafisa wa uchaguzi nchini Lesotho wanachunguza kwa nini maafisa walio na silaha walipelekwa kwenye vituo vingi vya kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu uliofanywa siku ya jumamosi.Hatibu wa tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo Tuoe Hantsi aliwambuia wanahabari kuwaA� taifa zima,wapiga kura na hata swaangalizi w uchaguzi huo walitamaushwa na hatua hiyo,huku wakihisi badhi ya wapiga kura walitishika kutokana na uwepo wa maafisa wengi wa kijeshi.Alisema sheria iko bayana kuhusu ni mafias gani wanaostahili kuwepo kwenye vituo vya kupigia kura na kwamba kuwepo kwa askatri jeshi walio na silaha kulisababisha hofu miongoni mwa wapiga kura.Uchaguzi wa siku ya jumamosi ulikuwa kinyanga��anyiro kikubwa kati ya wapinzani wawili wa jadi Pakalitha Mosisili na Thomas Tabane,ambao wote washahudumu katika washifa wa waziri mkuu.Thabane alitoroka kutoka nchini humoA� mwaka waA� 2014 wakati kulipotokea mapinduzi ya kijeshi alipokuwa mamlakani.Kwa mujibu wa wachanganuzi wa maswala ya kisiasa huenda Mosissili akashinda uchaguzi huo.Mara nyingi jeshi la nchi hiyo limeshutumiwa kwa kuingilia shughuli za uchaguzi mkuu katika taifa hilo lisilo na bandari na klenye jumla ya idadi ya watu milioni 2.Mnamo miaka ya hivi majuzi Lesotho imekabiliwa na visa kadhaa vya majaribio ya kuipindua serikali na utepetevu wa kisiasa.