NTSA yaonya wananchi dhidi ya kushambulia maafisa wake

Halmashauri ya kitaifa kuhusu usalama barabarani (NTSA) imewaonya wananchi dhidi ya kuwashambulia maafisa wake wakati wa msako dhidi ya madereva wanaoendesha magari wakiwa walevi. Haya yamejiri baada ya baadhi ya maafisa wa NTSA kushambuliwa kwa mawe walipokuwa wakitekeleza operesheni dhidi ya madereva walevi jijini Nairobi, hatua ambayo mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyo Francis Meja amesema haitavumiliwa. Alisema hali hiyo imetokana na hali ya kufasili visivyo maswala kuhusiana na uamuzi uliotolewa hivi maajuzi na mahakama ya rufani ambao miongoni mwa maswala mengine ulizungumzia matumizi ya vifaa vya kupima viwango vya ulevi vya madereva.A� Meja alikariri kwamba uamuzi huo haukupiga marufuku vifaa hivyo ila uliishauri halmashauri hiyo kutumia vifaa hivyo kubainisha tu iwapo mtu amelewa bila kuvitumia kama ushahidi mahakamani.

 

A�