Maafisa wa mahakama wapokea mafunzo ya rufaa za uchaguzi

Maafisa zaidi wa idara ya mahakama kutoka eneo la North Rift wamepata mafunzo kuhusu jinsi ya kushughulikia rufaa za uchaguzi ambazo huenda zikaibuka baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi Agosti . Kaimu jaji mkazi wa Eldoret Cecilia Githua alisema kuwa mpango huo wa mafunzo ni sehemu ya mipango ya awali inayolenga kuwapa maafisa hao wa idara ya mahakama mbinu za kushughulikia rufaa zitakazowasilishwa . Pia alisema kuwa jaji mkuuA� David Maraga anatarajiwa kuchapisha majina ya maafisa wote wa idara ya mahakama watakaoshughulikia rufaa za uchaguzi katika muda wa wiki mbili zijazoA� na kuongeza kuwa idara ya huduma za mahakama pia zitachapisha mahakama zote zitakazoshughulikia rufaa hizo za uchaguzi . Akiongea wakati wa hafla ya umma katika mahakama kuu ya Eldoret hii leo iliyoandaliwa na tume ya kimataifa ya majaji , jajiA� Githua alidokeza kuwa kesi zote ambazo bado ziko mahakamani huenda zikachelewa baada ya uchaguzi mkuu kwakuwa mahakama zitatilia mkazo rufaa za uchaguzi.