Maafisa wa halmashauri ya NEMA wakamata watu 10 wakiuza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku

Maafisa wa Halmashauri ya kitaifa ya Mazingira (Nema) wamewakamata watu 10 mjini Bomet waliokuwa wakiuza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku. Afisa mkuu mtendaji wa Nema huko Kisii, Tom Togo, alisema msako wao sasa umefikisha 19 watu waliokamatwa mwishoni mwa wiki baada yaw engine tisa kukamatwa siku ya Jumamosi katika miji ya Kisii na Keroka. Togo alisema washukiwa hao watafikishwa mahakamani siku ya jumatatu kwa kupuuza marufuku hiyo ya mifuko ya plastiki. Alisema pia wanalenga watu binafsi ambao bado wamehodhi mifuko ya plastiki na kuiuza wakati wa usiku. Togo said they have stepped up operations to ensure 100 percent compliance with the law.