Maafisa Wa EACC Wavamia Nyamira

Maafisa wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi walivamia afisi za serikali ya kaunti ya Nyamira na kuchukua komputa na faili zinazoaminika kuwa na habari muhimu kuhusu kesi ya ufisadi wanayofuatilia. Maafisa hao wa uchunguzi walichukua vifaa hivyo kutoka afisi za bodi ya utumishi wa umma ya kaunti hiyo pamoja na idara ya maswala ya jinsia na michezo vinavyoaminika kuwa na habari muhimu kuhusu uajiri tata wa wa maafisa-56 katika idara hiyo. Uajiri wa maafisa hao uliibua hisia kali tangia mwezi disemba, hali iliyosababisha bodi hiyo kubatilisha hatua hiyo. Idara hiyo pia ni miongoni mwa zile zinazoshutumiwa kwa ufujaji wa pesa.A�Kwengineko maafisa wa tume ya EACC waliwakamata maafisa watatu wa uhamiaji katika kituo cha Namanga kwenye mpaka baina ya Kenya na Tanzania kuhusiana na madai ya ufisadi.A�A�Maafisa haoA�walikamatwa kwa madai kwamba wanamiliki kituo binafsi cha kubadilishia fedha za kigeni ilihali huduma hizo zinapaswa kutolewa na idara hiyo. Maafisa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Namanga wakisubiri kufikishwa mahakamani.