Mwenyekiti Wa EACC Philip Kinisu Ahojiwa Na CID

Mwenyekiti wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Philip Kinisu ameandikisha taarifa na idara ya upelelezi wa jinai CID kuhusu madai ya kuhusishwaA� kwa biashara ya familia yake kwenye shughuli za ufisadi na mashirika mbali mbali ya serikali.A� Kinisu amehojiwa kwa saa kadhaa ambapo ametoa maelezo kuhusu jinsi kampuni ya familia yake ambayo ni Esaki Limited, ilivyoshinda zabuni ya serikali ya kusambaza bidhaa kwa shirika la vijana wa huduma kwa taifa NYS.A� Shirika la NYS linachunguzwa kuhusiana na shughuli za kutiliwa shaka za usambazaji bidhaa baada ya kubainika kuwa shirika hilo lilipoteza takriban shilingi milioniA� 800 zilizolipwa kampuni zisizojulikana kwa huduma ambazo hazikutolewa.