Maafisa wa chama cha madaktari wafika mbele ya kamati ya bunge

Maafisa wa chama cha madaktari wamefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu afya. Maafisa hao wametoa wito kwa bunge kuingilia kati kutatua mzozo unaokumba sekta ya afya hapa nchini. Madaktari hao wanaishutumu wizara ya afya kwa kuhujumu mashauriano yanaoendelea kwa kufichua yale yanayosemwa faraghani. Aidha wamedai hakuna uelewano baina ya waziri wa afyaA�A�Dr. Cleopa Mailu na katibu wa wizara hiyo Dr. Nicholas Muraguri. Mashauriano kuhusu mzozo huo yanadaiwa kuendelea vyema isipokuwa suala la nyongeza ya mshahara ambapo serikali inapendkeza nyongeza ya asilimia 40. Aliyekuwa katibu wa wizara hiyo Mark Bor pia amefika mbele ya kamati hiyo kuangazia kwa nini mkataba wa maelewano kati ya serikali na madaktari hao haukusajiliwa. Aidha kamati hiyo itakutana na baraza la magavana leo alasiri.