Maafisa wa AMISOM waimarisha operesheni dhidi ya Al-Shabaab

Maafisa wa KDF wanaohudumuA� chini ya kikosi cha muungano wa Afrika nchini SomaliaA� AMISOM wameimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab katika eneo la Gedo nchiniA� Somalia . Operesheni hiyo yaA� hivi punde iliyotekelezwa katika kambi moja ya wanamgambo katika eneo la Kataama huko Gedo takriban kilomita 104 kutoka mji wa mpakani wa Elwak imesababisha mauaji ya wanamgambo 15. Kambi hiyo iliharibiwa wakati wa operesheni hiyo. Wanamgambo wangine kadhaa walijeruhiwa huku mfumo wao wa mawasiliano ukiharibiwa. Msemaji wa vikosi vya KDF Joseph Owuoth amesema operesheni hiyo itaendelea hadi wanamgambo wote wa kundi la Al-qaeda waangamizwe.