Maafisa Wa Afya Ya Umma Wanasa Kilo 200 Za Nyama Isiyokaguliwa Nakuru

Maafisa wa huduma ya afya kwa umma huko Nakuru jana walinasa zaidi ya kilo 200 za nyama ambayo haijakaguliwa,ilipokuwa ikipakuliwa nje ya duka moja la kuuza nyama mjini humo.Afisa wa afya ya umma katika kaunti hiyo Samwel Kinga��ori alisema kuwa nyama hiyo ilitoka mjini Elburgon,katika kaunti ndogo ya Molo na kuongeza kuwa uchunguzi umeshaanzishwa ili kubaini yule aliyekuwa akisafirisha nyama ambayo haijakaguliwa bila leseni.Alisema visa kama hivyo vimesharipotiwa katika sehemu hiyo katika mwezi mmoja uliopita,hali ambayo inahatarisha afya ya umma.Kinga��ori alisema kuwa kaunti hiyo imo mbioni kubuni sheria za kudhibiti uuzaji wa nyama katika kaunti hiyo.Chini ya sheria hiyo mpya magari yote ya kusafirisha nyama yatalazimika kuwa na leseni na kuwekwa vibandiko maalum.