Mifugo Waangamia Kutokana Na Kiangazi Marsabit

Huku hali ya kiangazi ikiendelea kukithiri katika maeneo mengi humu nchini,asili mia 80 ya mifugo katika lokesheni ya Ngalas eneo bunge laA� North Horr kaunti ya Marsabit wameripotiwa kuangamia kutokana na njaa.Chifu wa sehemu hiyo Mata Sora,amedhibtisha tukio hilo akiongeza kwamba hali hiyo inaendelea kuzorota kila uchao na watu wanaotegemea mifugo kujikimu kimaisha, sasa wanahitaji msaada wa dharura wa chakula. Chifu Sora aliongeza kuwa hakuna mtu aliyefariki kufikia sasa kutokana na hali hiyo ya ukame na njaa.

Hata hivyo wakaazi wa sehemu hizoA� Bone Chachu naA� Elema Eli wanadai kuwa wakongwe saba wamepoteza maisha yao kutokana na njaa.

Chachu aliongeza kuwa zaidi ya mbuzi wake 300 wamefariki na sasa amelazimika kuwalisha mbuzi waliosehemu ya msaada wake wa chakula.Baadhi ya wakazi sasa wamehama pamoja na mifugo wao hadi Ethiopia kutafuta lishe.Mashirika yasiyo ya kiserikali katika sehemu hiyo yameonya kuwa mifugo pamoja na watu zaidi huenda wakapoteza maisha yao endapo hatua hazitachukuliwa.

A�

A�

A�