Louis van Gaal ashawishi Daley Blind kujiunga na Old Trafford

Kocha wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amemshawishi Daley Blind kutuma ombi la kuondoka Old Trafford na kujiunga na Barcelona.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi hajachezeshwa katika siku za hivi majuzi licha ya uwezo wake wa kucheza katika nafasi nyingi. Aidha, Van Gaal aliilaumu vikali Machester United baada ya kutimuliwa mwaka 2016. Blind amecheza mechi moja pekee tangu mwezi Septemba jambo linalomkera Van Gaal. Hata hivyo, United huenda ikaamua kumwongeza kandarasi ya miezi kumi na miwili hadi mwaka 2018.