Ligi ya taifa a�?Supera�� kuanza tarehe 10 mwezi Februari

Msimu wa ligi ya taifa a�?Supera�� utaanza tarehe 10 mwezi Februari. Kulingana na ratiba iliyotolewa na shirikisho la soka humu nchini jumla ya mechi sita zitachezwa katika siku ya kwanza ya ligi hiyo. Timu zilizoshushwa ngazi kutoka ligi ya Sportpesa humu nchini Muhoroni Youth FC na Western Stima FC zitaanza kampeini ya kuwania ubingwa katika ligi ya taifa ya Super kwa mechi dhidi ya KCB FC na Modern Coast Rangers FC mtawalia. Ushuru FC iliyoshindwa kujikatia tikiti ya kushiriki ligi ya Sportpesa baada ya ushinde wa jumla ya mabao mawili kwa moja na Thika United itajitosa ugani dhidi ya Administration Police FC. Timu nyingine iliyoshiriki katika ligi hii, Nakuru Allstars itanuia kujiimarisha msimu ujao baada ya kumaliza katika nafasi ya tisa msimu wa mwaka 2015. Timu hiyo itaanza kampeini yake kwa mechi dhidi ya Isbania. Katika msimu wa mwaka 2017, timu za Mosca FC na Agro Chemical FC zilishushwa ngazi baada ya kumaliza katika nafasi mbili za mwisho kwa alama 15 na 28 mtawalia na sasa zitashiriki kwenye ligi ya divisheni ya kwanza ya FKF mwaka 2018.