Ligi ya mabingwa Barani Ulaya kunga��oa nanga leo usiku

Mechi za ligi ya mabingwa Barani Ulaya zitanga��oa nanga leo usiku, huku timu mahiri Barani humo zikimenyana. Juventus, iliyopoteza fainali msimu uliopita, itaelekea uwanjani a�?Camp Noua�? kuchuana na Baselona, marudiano ya mchuano wa robo fainali msimu uliopita, huku Waitaliano wakishinda kwa jumla ya mabao matatu kwa bila. Timu hizo zinatarajiwa kufuzu kundini ingawa mechi za nyumbani na ugenini zitaamua atakayeongoza kundini. Timu hizo zilipoteza wachezaji muhimu, huku Neymar akihamia PSG kutoka Baselona, naye Leonardo Bonucci akiondoka jijini Turin kujiunga na AC Milan. Katika mechi nyingineA� leo usiku; Celtic itaikaribisha PSG nchini Uskoti, mbingwa wa Ujerumani Bayern Munich watacheza na Anderlecht, Chelsea itatoana jasho na Qarabag FK na Olympiakos itamaliza udhia na Sporting Lisbon. Aidha,timu yaA� Roma itapambana na Atletico Madrid, CSKA Moscow iko nchini Ureno kumenyana na Benfica, nayo Manchester United itaialika Basel uwanjani Old Trafford.