Liberia kuandaa duru ya pili ya uchaguzi

Liberia sasa itaandaa duru ya pili ya uchaguzi wake wa urais tarehe 26 mwezi huu,kulingana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo. Mwenyekiti huyo Jerome Korkoya aliongeza kwamba kampeini zitaanza mara moja na zinatarajiwa kutatamishwa tarehe 24 mwezi huu.Aliyekuwa nyota wa kandanda George Weah atakabiliana na makamu wa rais wa nchi hiyo Joseph Boakai kwenye uchaguzi huo uliocheleweshwa na rufaa iliyowasilishwa mahakamani na mgombeaji mmoja aliyekuwa watatu baada ya duru ya kwanza.Mshindi wa uchaguzi huo utachukua mahala pa rais Ellen Johnson Sirleaf.Mahakama ya juu nchini humo wiki jana alitupilia mbali rufaa hiyo ya Charles Brumskine wa chama cha Liberty aliyedai kulikuwa na kasoro nyingi kwenye uchaguzi huo.