KWS yaeleza hisia zake kufuatia ongezeko wa visa vya biashara ya nyama mwitu

Shirika la huduma kwa wanyama pori KWS limeelezea hisia zake kufuatia kuongezeka kwa visa vya biashara ya nyama mwitu huko Naivasha na Gilgil katika muda wa miezi miwili iliyopita.Hayo yanajiri huku maafisa wa mashirika ya umma wakiwanasa washukiwa wawili pamoja na zaidi ya kila mia moja za nyama ya punda mlia katika kijiji cha Nagum huko Gilgil. Kisa hicho kinatokea siku moja baada ya washukiwa wengine wanane kutiwa nguvuni katika shamba jirani la Ol-Morogi baada ya kuwauawa punda milia saba na swara mmoja.Akaiongea kwa njia ya simu,Hapicha Ellema afisa mkuu wa mbuga ya wanyama ya Hellsgate alisema washukiwa hao wawili walishtakiwa mahakamani.Alilalamikia kukithiri kwa biashara ya nyama mwitu huko Naivasha na Gilgil akiongeza kuwa zaidi ya washukiwa 30 wametiwa nguvuni na kushtakiwa mwaka huu.Afisa huyo alisema maeneo ambapo biashara hiyo imekithiri zaidi ni yale ya Kigio, KARI, Kenya Nut farm, Suswa na Marula .Kulingana na Ellema, biashara hiyo haramu sasa imepenyeza hadi miji ya Nairobi na Nakuru.