KUSU Na UASU Kujiunga Na Madaktari Katika Mgomo

Huku serikali ikitafakari masharti ya matakwa ya madaktari ya nyongeza ya mshahara, wahadhiri na wahudumu wengine wa vyuo vikuu vya umma wametishia kugoma wakitaka kutekelezwa pendekezo mbadala la makubaliano ya pamoja ambayo hayajatekelezwa. Wametoa ilani ya mgomo ya siku saba kushinikizaA� masharti bora zaidi lichaA� ya kuongezeka gharama ya ulipaji mishahara. Chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu-UASU na kile cha wahudumu wa vyuo vikuu KUSU zilitoa ilani hiyo baada ya kutibuka mashauri ya kusuluhisha zogo kuhusu makubaliano ya pamoja ya nyongeza ya mshahara. Jana waliaanda mkutano na kundi la wapatanishi wakiongozwa na naibu Vice-chancellor Isaac Mbeche lakini hakukuwa na pendekezo mbadala. Katibu mkuu wa kitaifa wa chama cha UASU Constantine Wasonga na mwenzake wa chama cha KUSU Charles Mukhwaya waliviambia vyombo vya habari jijini Nairobi kwamba kushindwa kwa serikali kuwasilisha pendekezo mbadala kwa lile la mwaka 2013 kuna nia mbaya.A� Waliongeza kusema kwamba mgomo uliopangwa utaathiri vyuo vikuu 33 vya umma. Kwenye taarifa, waliikosoa serikali kwa kuto-zingatia mashauri ya kusuluhisha zogo hilo. Wawili hao walisema wahadhiri walipokea nyongeza ya mshahara mwaka wa 2010.A� Ilani hiyo ya mgomo imetolewa huku mashauri yakitibuka kati ya chama hicho na wasimamizi wa vyuo vikuu. Mukhwaya alionya kwamba ikiwa serikali haitazingatia mashauri basi ijitayarishe kwa mgomo huo unaotokota.