Kura za duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Liberia inaendelea

Shughuli ya kuhesabu kura za duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Liberia inaendelea siku moja baada ya uchgauzi huo ulioendeashwa kwa amani na ambao wapiga kura wanatarajia utachaangia mpito wa kidemokrasia katika muda wa zaidi ya miaka 70 nchini humo. Matokeo yanatarajiwa kutangazwa katika muda wa siku chache. Kura hiyo iliyocheleweshwa ilipigwa jumanne na ilihusisha George Weah, mwakandanda wa zamani wa kimataifa wa umri wa miaka 51 ambaye pia ni seneta dhidi ya Joseph Boakai mwenye umri wa miaka 73 ambaye amekuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo kwa miaka 12 sasa. Takriban watu milioni 2.2 wamesajiliwa kupiga kwenye duru ya pili ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi. Weah, ambaye alishinda kwenye duru ya kwanza hakupata asili-mia 50 inayohitajika kumtangaza mgombeaji wa urais kuwa mshindi ana matumani makubwa ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi huo. Hata hivyo, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni ndogo ikilinganishjwa na wale walioshiriki duru ya kwanza.