Kura ya mashtaka dhidi ya rais wa Brazil aliyesimamishwa kazi Dilma Rousseff…

dilma3
Kamati ya mashtaka ya bunge la Senate nchini Brazil imepiga kura ya kumfungulia mashtaka rais wa Brazil aliyesimamishwa kaziA�A�Dilma Rousseff kwa kukiuka sheria za bajeti. Hali hii inafungua mchakato wa kumwondoa afisini rais huyo. Kamati ya wanachamaA�A�21 ilipiga kura kwa kauli moja kumfungulia mashtaka Rousseff kwa kufuja akaunti za serikali ili kuruhusu matumizi zaidi ya pesa za umma katika mchakato wa kutaka kuchaguliwa tena mwaka waA�A�2014. Kuondolewa kwa rais huyo mamlakani kutatamatisha uongozi wa miaka 13 wa chama cha mrengo wa kushoto kati cha Workers Party.A�A�Utawala wake umegubikwa na kashfa kadhaa za ufisadi na kusababisha mzozo mbaya zaidi ya kisiasa katika taifa hilo ambalo lonaandaa michezo ya Olimpiki. Msukosuko wa kisiasa umewafanya viongozi wengi wa kisiasa kususia michezo hiyo ambayo inafunguliwa rasmi hivi leo.