Kundi la Mao lakabiliwa na maafisa wa usalama India

Yamkini wanamgambo 16 wa kundi la Mao waliuawa wakati wa makabiliano na maafisa wa usalama nchini India. Tukio hilo lilijiri mahali ambako wanamgambo waliwaua maafisa kadhaa wa usalama mwezi uliopita. Zaidi ya maafisa 300 wa usalama wamekuwa wakiwasaka wanamgambo hao katika wilaya ya Bijapur, jimbo la Chhattisgarh ambako wanamgambo hao wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa serikali kwa zaidi ya miaka 50. Haikubainika mara moja wakati mapigano hayo yalipotokea ingawa afisa mmoja wa polisi alidokeza kuwa wanamgambo hao waliuawa kwenye visa viwili tofauti vya ufyatulianaji risasi na mafisa wa usalama na kwamba afisa mmoja wa polisi aliuawa wakati wa tukio hilo.