Kundi la ISIS lasalia kuwa tisho kubwa kwa uhuru wa kuabudu ulimwenguni

Utawala wa raisA� Donald Trump umesema kuwa kundi laA� Islamic State of Iraq and Levant ambalo linafahamika kama ISIL au ISIS linasalia kuwa tisho kubwa zaidi kwa Uhuru wa kuabudu ulimwenguni. Idara ya maswala ya nje ya Marekani imesema kuwa mauaji ya wafuasi wa makundi ya Yazidis, wakristo na waislamu wa kishia na wafuasi wa kundi hilo la ISIL ni sawa na mauaji ya halaiki. Ripoti moja ya kila mwaka inasema kuwa takriban asilimia 80 ya idadi ya watu ulimwenguni inaendelea kuishi kwa hofu na kutatiza Uhuru wao wa kuabudu. Mataifa yanayolaumiwa zaidi ni mshirika wa Marekani,A� Saudi Arabia naA� Bahrain.