Kuna usalama wa kutosha, Matiang’i

Kaimu waziri wa usalama wa kitaifa Dkt Fred Matiang’i amewahakikishia wakenya kuweko kwa usalama huku wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Waziri huyo alisisitiza kujitolea kwa serikali kuhakikisha kuwa nchi hii ni salama . Matiangi pia alitoa wito kwa wakenya kujiepusha na vitendo ambavyo huenda vikahatarisha maisha yao na ya wenzao na kutatiza nchi hii . Waziri huyo aliyehutubia wanahabari na kuandamana na mwanasheria mkuu Githu Muigai na waziri wa ulinzi Raychelle Omamo aliwahimiza wananchi kuwa na ukomavu wanapowasiliana kupitia mitandao ya kijamii.