Kuapishwa kwa naibu gavana kaunti ya Nyeri kumeahirishwa

A�Mipango ya kumuapisha naibu gavana wa kaunti ya Nyeri, Mutahi Kahiga kuwa gavana wa kaunty hiyo alhamisi ijayo imeahirishwa kwa muda usiojulikana.Kahiga alitarajiwa kuapishwa kesho alaasiri kuwa gavana wa nne wa kaunty ya Nyeri kufuatia kifo cha gavanaA� Wahome Gakuru.Kulingana na maafisa wakuu wa serikali yak aunty hiyo wakiongozwa na afisa mkuu wa uchukuzi, miundo msingi na ujenzi,Muthui Kariuki,ipo haja ya kuwa na gavana wa kaunty hiyo afisini ili kuwezesha shughuli za kaunty hiyo kuendelea kama kawaida.Kuhusu ni nani atakayekuwa naibu wa Mutahi endapo atachukua hatamu za gavana wa kaunty hiyo,mshauri wa kisheria wa kaunty ya Nyeri Mwangi Mugo,anasema sheria kuhusu utawala wa kaunty hazisemi lolote kuhusu uteuzi kama huo.Alisema gavana mpya huenda akahudumu kwa kipindi kilichosalia bila naibu wake endapo sheria hiyo hitabadilishwa.