Kuapishwa kwa mtu asiyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi ni uhaini ;Githu

Mwanasheria mkuu prof. Githu Muigai amesema kuwa kuapishwa kwa mtu yeyote ambaye ahajatangazwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi wa urais wa hivi maajuzi uliotekelezwa na tume ya IEBC ni kinyume cha sheria na ni uhaini. Alisema kuwa serikali haijafahamishwa kuhusu sherehe yoyote ya upaishaji na muungano pinzani wa NASA huku akionya kuwa yeyote atakayeshiriki kwenye sherehe hiyo mbadala atachukuliwa hatua za kisheria. Akiwahutubia wanahabari leo asubuhi alsiema kuwa bunge la wananchi la muungano huo ni kinyume cha sheria na kuonya kaunti zinazotumia pesa za umma kufadhili hoja kama hizo kwamba ziwe tayari kuwajibika. Alisema kwua wale wanaoshinikiza kubuniwa kwa taasisi za bunge la wananchi wanapuuza sheria na wanadharau mahakama.