Kuapisha Raila ni chanzo cha ghasia, Alfred Mutua

Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na hafla iliyopangwa ya kuwaapisha vinara wa muungao wa NASA Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, na kutaja hatua hiyo kuwa chanzo cha ghasia. Mutua alisema kuwa nchi hii haiwezi kuwa na marais wawili na kuongeza kuwa wakenyaA� wanapaswa kujiuliza maswali kuhusu mustakabali wa nchi hii. Katika akaunti yake yaA�mtandao wa twitter, Dkt. Mutua alisema kuwa siasa zinapaswa kuendelezwa ili kuafikia maendeleo na sio kuwafukuza wawekezaji. Alisema hafla hiyo ya kuapisha huenda ikaitumbukiza nchi hii katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Alisema kuwa nchi hii tayari iko na rais na shughuli za serikali za kaunti pia zinaendelea.