KPL Allsters yarazwa mambao 4-0 na Cordoba FC Uhispania

Timu ya daraja la pili nchini Uhispania ya Cordoba FC iliicharaza timu ya KPL Allstars ya humuA� nchini mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana usiku nchini Uhispania. Timu hiyo inajumuisha wachezaji waliochaguliwa kutoka timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligiA� kuu nchini ya soka ya Sportpesa. Timu hiyo itacheza na timu ya Sevilla atletico siku ya jumamosi. Kwingineko, Mlindalango wa Arsenali Wojciech Szczesny amekamilisha uhamisho wake wa pauni milioni kumi hadi Juventus. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na saba aliyeichezea Roma kwa mkopo kwa miaka miwili ametia saini kandarasi ya miaka minne na mabingwa hao wa soka nchini Italia. Aidha, mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland aliichezea Roma mechi thelathini na nane msimu uliopita huku akikosa kufungwa katika mechi kumi na nne. SzczesnyA� atangangania nafasi na mlindalango mzoefu Gianluigi Buffon. MchezajiA� huyo aliruhusiwa kuondoka uwanjani Emirates baada ya kuwasili kwa mlindalangoA� Petr Czech.