Kongamano La Kimataifa La Sita Kuhusu Maendeleo Ya Afrika

TICAD-Uhuru-

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni na biashara ya kimataifa balozi Amina Mohamed amesema kwamba Kenya itakuwa mwenyeji wa kongamano la sita la kimataifa la Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (TICAD VI) kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu jijini Nairobi. Waziri Amina Mohamed alisema kukiwa na mipango mbali mbali ya (TICAD) ambayo tayari inaendelea kote barani Afrika, kongamano hilo litakuwa fursa nzuri ya kutizama changamoto na pia fursa zilizopo katika juhudi za kufanikisha ajenda ya (TICAD).

Waziri Amina MohamedA� alikuwa akihutubu wakati wa kukabidhiwa na waziri wa utalii Najib Balala- makao makuu ya kongamano la (TICAD), kwenye jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta – (KICC), mahala ambako pataandaliwa kongamano hilo. ambayo Zoezi ambalo litatanguliwa na shughuli kadhaa muhimuA� katika Jiji la nairobi ambapo takribani kampuni 100 za kibinafsi kutoka Japan na pia barani Afrika zitaonyesha bidhaa zao, hivyo kutoa fursa kwa wafanyibiashara wa bara hiliA� kuafikia mikataba.

Wajumbe elfu-4, kutoka Japan na zaidi ya elfu-6, kutoka kwa kampuni za Ki-Afrika na nyingine kutoka pembe zote za dunia wanatarajiwA kuhudhuria. Hii itakuwa mara ya pili ambapo Kenya imechaguliwa taifa la kwanza barani Afrika kuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya kimataifa, yaani mkutano wa shirika la biashara dunianiA� (WTO) na ule wa (TICAD VI).Kenya ni nchi ya kwanza kuwa mwenyeji wa kongamano la TICAD nnje ya Japan, mpango ambao ulizinduliwa na serikali ya Japan mwaka 1993.