Kombe la dunia la piga kambi katika jumba la KICC

Taji ya Kombe la dunia iliyowasili humu nchini jana iko katika jumba la KICC alasiri hii kwa watu wanaotaka kuitazama.Kombe hilo limefinyangwa kwa karati za Dhahabu 18 huku sehemu ya chini ikitengenezwa kwa kito cha thamani kinachomeremeta.

Lina urefu wa sentimita 36.8 na uzani kilo 6.1. Kombe hilo liliundwa na kampuni ya Stabilimento Artistico Bertoni nchini Italia, mwaka 1974. Kombe hiloA� litapelekwa nchini Msumbiji kesho kisha lielekee Uganda, Naijeria na Misri. Kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil lilitwaliwa na timu ya soka ya Ujerumani baada ya kuishinda Ajentina bao moja kwa bila fainalini kwenye muda wa ziada nchini Brazil. Mwaka huu fainali za kombe la dunia zitakuwa katika makala yake ya 21, kuanzia tarehe 14 mwezi Juni hadi 15 mwezi Julai. Mwaka huu Bara la Afrika litawakilishwa katika fainali hizo na mataifa matano: Naijeria, Misri, Tunisia, Moroko na Senegali.