Kocha wa Fulham hatarini iwapo hatashinda mechi mbili zijazo

Kocha wa kilabu cha Fulham kinachoshiriki kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza Slavisa Jokanovic atapigwa kalamu na kilabu hicho iwapo hatanyakua ushindi katika michuano miwili ijayo ya timu hiyo.Jokanovic aliyeiongoza timu hiyo kupandishwa ngazi hadi ligi kuu ya soka Uingereza ana kibarua kigumu sasa cha kuisaidia Fulham kunyakua ushindi baada ya timu hiyo kukosa kuandikisha ushindi tangu mwezi Agosti.

 

Timu hiyo ilishindwa na Cardiff mabao manne kwa mawili mwishoni mwa juma lililopita na ilikuwa imeshindwa na Asenali mabao matano kwa moja na mabao matatu kwa nunge na Everton. Fulham inashikilia nafasi ya 18 kwenye msururu wa ligi kwa alama tano ambapo itajitosa ugani kwa mechi Jumamosi hii dhidi ya Bournemouth kisha ichuane na mabingwa watetezi Manchester City.