Kocha Mkuu Wa Timu Ya Taifa Ya Nigeria “Super Eagles” Ajiuzulu

Sunday Oliseh amejiuzulu kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria almaarufu a�?Super Eaglesa��, miezi saba tu baada ya kuteuliwa. Oliseh, aliyetangaza kujiuzulu kwake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter alisema kuwa alichukua hatua hiyo kufuatia kukiukwa kwa mkataba wake na shirikisho la soka nchini humo, NFF. Oliseh ambaye aliteuliwa kwa mbwembwe na shirikisho hilo alianza kukabiliwa na changamoto pindi tuu baada ya uteuzi wake huku akililalamikia marupurupu yake, mbinu na matokeo ya michuano. Malalamishi yake kuhusu kutolipwa mshahara wake hayakupokelewa vyema na kamati kuu ya shirikisho hilo iliyotishia kuchukua hatua dhidi yake. Kwanzia alhamisi Oliseh aliamuriwa kuripoti kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo ambaye pia ni mshauri wa ukufunzi wa shirikisho hilo Amodu Shuaibu. Shirikisho la soka la nchini humo halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na matukio hayo.