KNUT yataka serikali kuwaondoa walimu kutoka maeneo ya Garissa ,Mandela na Wajir kufuatia tisho la ugaidi

Chama cha kitaifa cha waalimu KNUT kimetoa wito kwa serikali iwaondoe mara moja walimu kutoka kaunty za Mandera, Garissa A�na wajir kwa kuhofia usalama wao. KNUT imesema wito huo unafuatia lile shambulizi la ijumaa ambapo walimu watatu waliuawa kwenye shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika shule ya msingi ya Qarsa.Akiongea na wanahabari mjini Wajir , katibu wa KNUT katika kaunty hiyo Noor Bardad alithibitisha kuondoka kwa walimu wengi kutoka eneo hilo huku akitoa mfano wa shule ya msingi na Secondary ya Khorof Harar , Wajir Bor, Riba, Sarman, Kutulo na Tarbaj kuwa baadhi ya shule ambazo zimeathiriwa na kuhama kwa walimu wengi. Alisema zaidi ya shule 15 A�za msingi zimeathiriwa na kuondoka kwa walimu kutoka maeneo mengine ya nchi ambao ni asilimia 60 ya walimu wanaohudumu katika kaunty ya Wajir.